Kenya -Uganda

Refarii wa kike wa Uganda kuchezesha kombe la Dunia, makocha 140 waomba kibarua Kenya

Refarii wa kike Diana Mkasa kutoka Uganda amealikwa kuchezesha michuano ya kombe la dunia kwa upande wa akina wanawake wasiozidi miaka 17 nchini Azerbaijan kati ya Septemba tarehe 22 hadi Oktoba tarehe 13.

Matangazo ya kibiashara

Mukasa ni mmoja wa Marefarii watatu, Amegee Aissata kutoka Togo na Aglago Emmanuella kutoka Ghana waliochaguliwa kutoka barani Afrika kuchezesha m,echi hizo ambapo marefarii 14 watashiriki katika michuano hiyo.

Katika hatua nyingine Shirikisho la Soka nchini Kenya, FKF linasema limepokea maombi 140 kutoka kwa makocha wa kigeni wanaotafuta kazi ya kuifunza timu ya soka ya nchi hiyo Haraambee Stars.

Miongoni mwa makocha hao waliotuma maombio ni pamoja na Oliver Page wa Ujerumani na Samson Siasia kutoka Nigeria.

Hata hivyo Elly Mukolwe mwenyekiti wa kamati ya kiufundi ya shirkisho hilo la soka anasema inasikitisha kuwa ni makocha watano tu kutoka Kenya ndio waliotuma maombi yao hadi sasa.

Kocha wa Harambee Stars Francis Kimanzi alifutwa kazi wiki iliyopita kutokana na matokeo mabaya ya tiimu ya soka ya Kenya.