UINGEREZA

Andre Villas-Boas ajigamba kufanya maajabu akiwa na Tottenham Hotspur

Kocha Mpya wa Tottenham Hotspur Andre Villas-Boas ambaye ameingia mkata wa miaka mitatu kwa ajili ya kikonoa kikosi hicho
Kocha Mpya wa Tottenham Hotspur Andre Villas-Boas ambaye ameingia mkata wa miaka mitatu kwa ajili ya kikonoa kikosi hicho

Kocha Mkuu wa Tottenham Hotspur Andre Villas-Boas ambaye amesini mkataba wa miaka mitatu kuinoa Klabu hiyo amesema atahakikisha analeta mapinduzi na kuifanikisha kuweza kumaliza katika nafasi tatu za juu kwenye msimu ujao wa Ligi.

Matangazo ya kibiashara

Villas-Boas ambaye alikuwa kocha wa zamani wa Chelsea kabla ya kuchukua mikoba ya Harry Redknapp ambaye ametimuliwa majuma matatu yaliyopita amesema ni lazima afanye vizuri ili kurejesha imani kwa uongozi.

Villas-Boas amewaambia wanahabari kuwa nafasi ya yeye kupewa kukinoa kikosi cha Tottenham ni kitu cha kipekee na atahakikisha anafanyakazi kwa kiwango chake chote na kuipa mafanikio Klabu hiyo.

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea aliyetimuliwa kutokana na timu yake kuwa na matokeo mabaya amesema Tottenham ina kikosi bora ambacho kila Kocha anahamu ya kukifundisha na kupata nacho mafanikio ya haraka.

Villas-Boas ameongeza kuwa kwa pamoja watahakikisha wanapata matokeo ambayo yamekuwa kiu kwa mashabiki wa Tottenham ambayo mara kadhaa imekuwa ikipoteza fursa ya kufanya vizuri mwishoni mwa msimu.

Mwenyekiti wa Klabu ya Tottenham Daniel Levy amesema wanamatumaini timu yao itafanya vizuri chini ya Kocha mpya Villas-Boas na ametaka wachezaji kumpa ushirikiano wa kutosha ili kutimiza malengo yake.

Villas-Boas mwenye miaka 34 akiwa anainoa klabu ya FC Porto alifanikiwa kutwa Ubingwa wa Europa ndiyo Chelsea ikavutiwa na huduma yake lakini akadumu kwa siku 256 kabla ya kitimuliwa Stamford Bridge.

Miongoni mwa makocha ambao walikuwa wanatajwa uwa warithi wa Redknapp ni pamoja na Kocha wa zamani wa Ufaransa Laurent Blanc, Kocha wa Wigan Roberto Martinez, Kocha wa zamani wa Uingereza Fabio Capello na Mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Jurgen Klinsmann.