Uingereza

Kesi ya John Terry dhidi ya Ferdinand yasikilizwa hii leo

John Terry, Mchezaji anayeshutumiwa kutumia Lugha ya kibaguzi uwanjani.
John Terry, Mchezaji anayeshutumiwa kutumia Lugha ya kibaguzi uwanjani. REUTERS/Stefan Wermuth

John Terry alitumia maneno yaliyoashiria Ubaguzi wa Rangi dhidi ya Rio Ferdinand wakati wa Mchezo wa mpira wa Miguu baada ya kufanyiwa kejeli juu ya shutma dhidi yake ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na aliyekuwa Mpenzi wa Mchezaji mwenzie. 

Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya Mjini Westminster nchini Uingereza hii leo imesikiliza kesi ya Terry akishutumiwa kutamka maneno ya kibaguzi wakati wa Mpambano wa Ligi kuu mwezi Oktoba Mwaka 2011.
Mwendesha Mashtaka katika Mahakama hiyo, Duncun Penny amesema Maneno ya

Terry yameonesha hali ya uadui na kumtenga kutokana na Rangi aliyonayo huku akisema kuwa huenda maneno hayo aliyatamka baada ya ishara alizozionesha Ferdinand juu ya Shutma za kuwa na uhusiano wa Kimapenzi na aliyekuwa Mpenzi wa Mchezaji mwenzie.
 

Terry alivuliwa unahodha wa Timu ya Taifa ya Uingereza na chama cha Soka nchini humo kutokana na Shutma za ubaguzi, hali iliyosababisha Kocha wa Timu ya Taifa ya Uingereza Fabio Capello kujiuzulu akioneshwa kutokubaliana na uamuzi huo.
Ikiwa atakutwa na Hatia Terry atatozwa Faini ya Mpaka EURO 3,850.