Uingereza

Mancini amwaga kalamu kuifundisha Mancity kwa Muhula wa Miaka mitano

Kocha wa Timu ya Mancity, Roberto Mancini
Kocha wa Timu ya Mancity, Roberto Mancini REUTERS/Phil Noble

Kocha wa Timu ya Manchester City, Roberto Mancini amekubali kutia saini Mkataba wa Miaka mitano na Mabingwa wa Ligi kuu nchini Uingereza, klabu hiyo imethibitisha.

Matangazo ya kibiashara

Mkataba huo utakaofanya kazi Mpaka kipindi cha Majira ya Joto ya Mwaka 2017 umekuja kufuatia mafanikio makubwa katika msimu uliokuja baada ya zaidi ya miongo minne kwa kuichapa Queens Park Rangers Mwezi May mwaka huu.
 

Man City ilinyakua ubingwa katika Mazingira ya Dakika za lala salama kutoka kwa Edin Dzeko na Sergio Aguero.

Mancini alirithi kibarua cha Mark Hughes mwezi Desemba mwaka 2009 na kuifanikisha City katika ligi ya FA.

Mancini ameisifu Manchester City kuwa timu madhubuti na amesema anategemea kufanya mengi mazuri akikabiliana na Changamoto zilizo mbele yake.