TANZANIA-RWANDA

Michuano ya kombe la kagame kutimua vumbi Dar es salaam,Tanzania.

Kikosi cha Yanga,kutoka nchini Tanzania
Kikosi cha Yanga,kutoka nchini Tanzania

Pazia la michuano ya Kagame linafunguliwa rasmi jumamosi ambapo takriban timu kadhaa zimewasili ijumaa nchini Tanzania na kukamilisha idadi ya timu kumi na moja zinazoshiriki mashindano ya Kombe la Kagame yanayoanza jumamosi katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Matangazo ya kibiashara

Mechi zinazoanza kushuka dimbani ni pamoja na APR ya Rwanda dhidi ya El Salam Wau ya Sudan Kusini itakayoanza saa 8 kamili mchana na kufuatiwa na ya saa 10 kamili jioni kati ya mabingwa watetezi Yanga na Atletico ya nchini Burundi.

Naye kocha mpya wa Yanga Tom Staintfiet raia wa Ubelgiji amesema hana shaka na kikosi chake ambacho amekuwa nacho kwa muda mfupi na kubaini uwezo mkubwa walionao wachezaji wake.

Aidha anaamini mechi itakuwa kali lakini anamatumaini ya kutoka na ushindi.