TANZANIA

Yanga yaanza vibaya michuano ya Afrika Mashariki na Kati.

Kikosi cha yanga kabla ya mchezo
Kikosi cha yanga kabla ya mchezo bongostaz.blogspot.com

Mashindano ya soka Afrika mashariki na Kati yamefunguliwa jana katika dimba la taifa jijini Dar es Salaam nchini Tanzania kwa mechi mbili ambapo katika mechi ya kwanza timu ya Wau salaam kutoka Sudan Kusini ikikubali kichapo cha magoli saba bila majibu 7-0 kutoka kwa APR ya Rwanda. 

Matangazo ya kibiashara

Katika mchezo wa pili baina ya Atletico ya Burundi na Young Africans ya Dar es Salaam Tanzania, kipindi cha kwanza kilimalizika huku timu hizo zikiwa bado hazijafungana lakini katika kipindi cha pili mambo yalibadilika na Yanga kujikuta ikikubali kipigo cha magoli mawili kwa nunge 2-0 huku goli la pili likifungwa katika dakika ya tatu ya muda wa ziada baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika.

Magoli ya Atletico yalifungwa na Olivier Ndikumana na kuipa ushindi timu hiyo katika mechi hii ya ufunguzi.

Kwa matokeo haya APR inashika nafasi ya kwanza katika kundi C ikifuatiwa na Atletico wakati mabingwa watetezi Yanga wanashika nafasi ya tatu na Wau Salaam ikishika nafasi ya mwisho.

Katika mchezo wa leo Simba ya Tanzania itavaana na UPR kutoka Uganda.