LONDON OLIMPIKI 2012

Caster Semeya asema yuko tayari kumenyana katika mbio za mita 800 wakati wa michezo ya Olmpiki

Bingwa wa dunia wa mbio za mita 800 kwa upande wa wanawake Caster Semenya raia wa Afrika Kusini, anasema hatatatizwa na kashfa ya 2009 kuhusu jinsia yake wakati aliposhinda mbio hizo za dunia na kunyakua nishani ya dhahabu.

Matangazo ya kibiashara

Semenya mwenye umri wa miaka 21 anafunzwa na bingwa wa mwaka 2000 wa mashindano ya Olimpiki Maria Mutola kutoka Msumbiji.

Bingwa huyo mwenye umri wa miaka 21 amesema amesahau matatizo yaliyomkumba mwaka 2009 na yuko tayari kabisa kupambana na wanaridha wengine wakati wa mashindano ya Olimpiki yanayoanza wiki ijayo jijini London Uingereza.

Mwaka huu Semeya ameweka muda bora wa dakika 1 sekunde 59 ikilinganishwa na Mkenya Pamela Jelimo .

Shirikisho la riadha duniani IAAF, ilimruhusu Semenya mwaka 2010  kuendelea kushiriki katika mashindano ya kimataifa baada ya kubainika kuwa hali yake ya kijinsia ni mwanamke.