CAF

Al Ahly na Zamalek kucheza bila ya mashabiki mjini Cairo

Klabu ya Al Ahly na Zamalek za Misri zitacheza kwa mara ya kwanza mwishoni mwa Juma bila ya mashabiki kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 10.

Matangazo ya kibiashara

Mechi hiyo itachezwa mjini Cairo bila ya mashabiki kwa sababu za kiusalama baada ya mauji ya mashabiki 74 mwezi Februari mwaka huu kati ya mashabiki wa Al Masry na Ahly mjini Port Said wakati wa kipindi cha mapinduzi ya kisiasa nchini humo.

Mechi hizo za kuwania nafasi ya kusonga mbele katika harakati za kuwania ubingwa wa klabu bora barani Afrika,taji ambalo Al Ahly limeshinda mara 11.

Aidha, Ahly inacheza na Zamalek wakiwa na rekodi nzuri ya kutoshindwa mara 12 dhidi ya wapinzani wao katika mechi za kimataifa.

Shirikisho la soka nchini Misri limepiga marufuku ligi kuu ya soka nchini humo kwa  kipindi cha miaka miwili ijayo kutokana na mauji ya mashabiki na sababu za kiusalama.

Hata hivyo, shirikisho la soka nchini humo limeruhusu mechi za kampeni za timu ya taifa kufuzu kwa kinyangayiro cha kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014 bila ya mashabiki.

Katika kundi A,  Etoile Sahel ya Tunisia na mabingwa watetezi Esperance  na ASO Chlef ya Algeria, Sunashine Stars ya Nigeria zitamenyana pia katika kampeni za kutafuta ubingwa huo.