SOKA-OLIMPIKI

Uhispania yaondolewa katika michezo ya Olimpiki

Timu ya taifa ya soka ya wanaume ya Uhispania imeondolewa katika michezo ya Olimpiki jijini London Uingereza.

Matangazo ya kibiashara

Mabingwa hao wa soka barani Ulaya waliwafungwa na Honduras bao 1 kwa 0 katika mchuano wa kundi D Jumapili.

Honduras sasa wamefuzu katika awamu ya pili pamoja na Japan baada ya kuifunga Morroco kwa bao 1 kwa 0.

Brazil nayo iliishinda Belarus mabao 3 kwa 1 katika mchuano wa kundi la C, huku Misri ikitoka sare ya bao 1 kwa 1 na New Zealand.

Katika mchuano mwingine wa kundi B, Mexico iliishinda Gabon kwa mabao 2 kwa 0 huku Korea Kusini ikiifunga Switzerland kwa mabao 2 kwa 1.

Brazil itakutana na Newzealand,Misri imenyane na Belarus huku Senegal ikicheza na Muungano wa Mmiliki za kiarbu siku ya Jumatano.

Michezo ya Olimpiki imeingia katika siku yake ya tatu jijini London na mashindano ya riadha yanatarajiwa kuanza siku ya Ijumaa ambapo mbio za kwanza za mita elfu tatu kuzuka maji na viunzi.