OLYMPIC-LONDON

Mwanariadha Usain Bolt afanikiwa kutetea ubingwa wake wa mita 100

Mwanariadha Usain Bolt akishangilia mara baada ya kushinda mbio za mita 100 hapo jana
Mwanariadha Usain Bolt akishangilia mara baada ya kushinda mbio za mita 100 hapo jana REUTERS/Paul Hackett

Mwanariadha Usain Bolt raia wa Jamaica amefanikiwa kutetea ubingwa wake wa dunia wa mita 100 kwenye mashindano ya Olympic baada ya kufanikiwa kuweka rekodi ya mashindano ya mwaka huu kwa muda wa sekunde 9.63.

Matangazo ya kibiashara

Bolt amefanikiwa kumaliza mbio hizo mbele ya mwanaridha mwenzake Yohan Blake na Mmarekani Justin Gatlin ambao awali kabla ya mbio hizo walitamba kumshinda mwanariadha huyo.

Wanariadha saba kati ya nane waliokimbia mbio hizo walifanikiwa kumaliza chini ya sekunde 10 na kuwa rekodi ya mashindano ya Olympic ya mwaka huu yanyofanyika jijini London.

Mara baada ya kushinda mbio hizo Bolt mwenyewe amesema kuwa alitarajia kufanya vizuri kwenye mbio hizo na kwamba alilenga kutetea rekodi yake ya dunia aliyoiweka miaka mitatu iliyopita nchini China.

Asafa Powell ambaye alitarajiwa kutoa upinzani mkali kwa Bolt alijikuta akimaliza wa mwisho kwa kutumia muda wa sekunde 11.99 na kushindwa kutimiza ahadi yake kuwa angemsinda Bolt.

Usain Bolt anatarajiwa pia kushirikia mbio za mita 200 na 400 ambpo iwapo atafanikiwa kushinda tena mbizo hizo ataweza kujinyakulia medali nyingine mbili za dhahabu baada ya kutwaa medali yake ya kwanza.