UINGEREZA

Van Persie asafiri na timu yake ya Arsenal kwenda Ujerumani licha ya kuhusishwa na kuihama timu hiyo

Robin Van Persie mshambuliaji wa Arsenal
Robin Van Persie mshambuliaji wa Arsenal Reuters

Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Robin Van Persie amesafiri na timu yake kuelekea nchini Ujerumani kwaajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya klabu ya Cologne licha ya kuwepo uvumi kuwa mchezaji huyo ana mpango wa kuihama klabu yake.

Matangazo ya kibiashara

Robin Van Persie ambaye anahusishwa na kutaka kuihama klabu yake ya Arsenal na kutakiwa na vilabu vya Juventus, Manchester City na Manchester Uinted ambazo zote kwa pamoja zimetuma maombi kwenye klabu hiyo kutaka kumsajili.

Kusafiri kwa mchezaji huyo na wechazaji wenzake huenda kukawa kunathibitisha kuwa mchezaji huyo atabakia kwenye klabu yake ya Arsenal licha ya kuhusishwa na kutaka kuihama klabu yake.

Hivi karibuni mchezaji huyo alitaka nyongeza ya mshahara toka kwa uongozi wa timu yake jambo ambalo lilizusha mjadala uliopelekea timu hiyo kutaka kumuuza Van Persie ambaye anaumri wa miaka 29 hivi sasa.

Mpaka sasa haijulikani iwapo mchezaji huyo ataendelea kusalia kwenye klabu hiyo au la kwakua hakuna mazungumzo mengine yoyote yanayoendelea kati ya mchezaji huyo na vilabu ambavyo vilikuwa vimetuma maombi kutaka kumsajili.