LONDON-OLYMPICS 2012

Brazil na Mexico kukutana kwenye fainali michuano ya Olympic

Javier Cortes mchezaji wa timu ya taifa ya Olympic ya Mexico akishangilia baada ya kuifungia timu yake goli la ushindi dhidi ya Japan
Javier Cortes mchezaji wa timu ya taifa ya Olympic ya Mexico akishangilia baada ya kuifungia timu yake goli la ushindi dhidi ya Japan Reuters

Michuano ya mpira wa miguu kwenye mashindano ya Olympic imeendelea hapo jana kwa baadhi ya miamba ya soka kutinga kwenye hatua ya fainali kuwania medali ya dhahabu.

Matangazo ya kibiashara

Kwenye mechi za hapo jana timu ya taifa ya Mexico ilifanikiwa kusonga mbele kwenye mashindano ya mwaka huu baada ya kuifunga timu ya taifa ya Japan kwa magoli 3-1 kwenye mchezo ambao Japan ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao.

Bao hili liliwafanya wachezaji wa Mexico kupata morali iliyopelekea kupata bao la kusawazisha na kisha kuongeza magoli mengine mawili yaliyoipatia ushindi timu hiyo.

Goli la Japan lilifungwa na Yuki Otsu wakati yale ya mexico yalifungwa na Mario fabian, Oribe Perelta na JaviersCortes.

Mchezo mwingine uliwakutanisha timu ya taifa ya Korea kusini waliokuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Brazil kwenye mchezo ambao ulishuhudia Brazil ikifanya mauaji kwa timu hiyo kwa kuifunga magoli 3-0.

Mabao ya Brazil yalifungwa na Romulo na mawili mengine yakifungwa na Da Silva dos Santos.