LONDON OLIMPIKI 2012

Mchezaji wa DRC aliyeripotiwa kupotea wakati wa Olimpiki azungumza

Mchezaji wa mchezo wa Judo Cedric Mandembo kutoka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambaye aliyeripotiwa kupotea wakati wa michezo ya Olimpiki jijini London Uingereza,ameibuka na kusema kuwa yupo mapumzikoni.

Matangazo ya kibiashara

Mandembo amesema kuwa yeye hakutoroka kambini na badala yake kusema muda wake wa kukaa nchini Uingereza unamalizika mwezi ujao na alikuwa ameamua kupumzika katika mji wa Manchester kabla ya kurejea nyumbani.

Watu wengine waliopotea ni pamoja na kocha wa mchezo huo wa Judo Ibula Masengo,mwenzake wa  ndondi Blaise Bekwa pamoja na kocha wa riadha Guy Nkita ambao hadi sasa hawajulikani waliko .

Waziri wa michezo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Baudoin Banza Mukalay, amesema ujumbe wa wanamichezo uliokwenda katika michezo hiyo na kushindwa kupata medali unawsili siku ya Jumatano.

Wachezaji wengine wa Cameroon pia waliripotiwa kupotea wakati wa michezo hiyo wakiwemo watatu kutoka nchini Cote Dvoire.

Visa vya wachezaji hasa wanariadha kupotea wakati wa michezo mikubwa kama ya Olimpiki vimekuwa vikiongezeka hasa kwa mataifa ya Afrika.