Uingereza

Ferguson awakosoa wachezaji baada ya kushindwa na Everton

Kocha wa Klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson amegeuka mbogo na kuwarushia makombora ya kuwakosoa wacheazaji wake kwa kushindwa kufurukuta mbele ya timu ya Everton na kukubali kipigo cha bao 1-0 ikiwa ni mechi yake ya kwanza kwenye kindumbwendumbwe cha ligi kuu ya Uingereza.

REUTERS/Christian Hartmann
Matangazo ya kibiashara

Kocha huyo amewalaumu wachezaji hao kwa kushindwa kutumia kipaji cha mchezaji nyota mpya Robin van Persie.

Robin van Persie aliingia dakika ya 68 na alitarajiwa kufanya maajabu lakini hali ilikuwa tofauti na kocha Sir Alex Ferguson kutumia mwanya huo kuwalaumu wachezaji wake baada ya kuambulia kipigo.

Mchezaji huyo ambaye alisaini mkataba wa paundi milioni 24 wa kujiunga na Manchester United iumaa iliyopita alishindwa kutia msukumo ndani ya timu hiyo katika mechi ya jana iliyokua kali huku Everton wakishambulia kwa nguvu.

Ferguson amesema kuwa timu yake ilishindwa kutumia fursa ambazo Van Persie huwa hafanyi makosa kwa kutumia uwezo wake wa kupenya lakini hawakumtumia vya kutosha kutokana na uzuri wake katika ufungaji.

Hata hivyo Ferguson ameelezea uamuzi wake wa kutomwanzisha mchezaji huyo katika kipindi cha kwanza na kusema kuwa alifanya hivyo kwa sababu Van Persie hakukaa muda wa kutosha na timu hiyo.