Jordan

Kocha wa Zamani wa Timu ya Taifa ya Misri aaga Dunia

Kocha wa Timu ya Taifa ya Misri, Mahmud al-Gohary aliyeifanikisha Timu yake kufuzu kuingia katika Mashindano ya Mpira wa Miguu ya Kombe la Miguu mwala 1990 ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 74.

Kocha wa Zamani wa Timu ya Taifa ya Misri
Kocha wa Zamani wa Timu ya Taifa ya Misri
Matangazo ya kibiashara

Al- Gohary alikuwa nchini Jordan ambako alikuwa akiugua akisumbuliwa na kiharusi ambacho kilishambulia Ubongo wake shirika la Habari la Misri MENA limeeleza.

Kocha huyo aliyeifanikisha timu ya Taifa ya Misri kwenda Italia kwa masindano ya Kombe la dunia, alipelekwa hospitalini Mjini Amman nchini Jordan ambako alikuwa akiifundisha Timu ya Taifa ya nchi hiyo.

Gohary aliwahi kuchezea Timu maarufu nchini Misri, Al Ahly kati ya mwaka 1955 na mwaka 1961, lakini majeraha yalimlazimu kukaa benchi.
 

Aliwahi kufundisha vilabu kadhaa ikiwemo Al Ahly na hasimu wake Zamalek, hali kadhalika alifundisha Timu ya taifa la Misri, Oman na Jordan.