Pata taarifa kuu
LIGI KUU YA UINGEREZA

Gerrard: waamuzi hawamtendei haki Luis Suarez

Mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez
Mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez Reuters
Ujumbe kutoka: Emmanuel Richard Makundi
1 Dakika

Nahodha wa klabu ya Liverpool, Steven Gerrard na beki Glen Johnson wamesema kuwa wanaimani kuwa waamuzi kwenye ligi kuu ya Uingereza hawamtendei haki mshambuliaji wa timu hiyo Luis Suarez.

Matangazo ya kibiashara

Wachezaji hao wameyasema hayo mara baada ya mchezo wao wa mwishoni mwa juma dhidi ya mahasimu wao klabu ya Manchester United kwenye mchezo ambao ulishuhudia timu hiyo ikizama kwa mabao 2-1.

Wameongeza kuwa mshambuliaji wao Luis Suarez aliangushwa mara kadhaa kwenye eneo la hatari lakini mwamuzi wa mchezo huo hakutaka kuizawadia timu hiyo penalt wala kutoa kadi ya njano kwa wachezaji wa Manchester Uinted.

Wachezaji hao wameenda mbali zaidi na kudai kuwa vitendo ambavyo vinafanywa na waamuzi hao sio vyakiungwana sababi inaonekana wanamchukia mchezaji huyo kutokana na kitendo chake cha ubaguzi wa rangi alichokifanya dhidi ya Patrice Evra.

Suarez mwenyewe alipoulizwa kuhusiana na mchezo huo hakusema chochote mbali na kudai kuwa suala la kutoa penalt au la linabaki kuwa ni lamwamuzi.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.