soka

Nigeria na Ghana zafuzu robo fainali kombe la dunia la wasichana wasiozidi miaka 17

Nigeria na Ghana zimefuzu katika hatua ya robo fainali ya michuano ya soka kuwania taji la dunia baina ya wasichana wasiozidi miaka 17, michuano inayoendelea nchini Azerbaijan.

Matangazo ya kibiashara

Nigeria ilifuzu katika hatua hiyo baada ya kumaliza ya kwanza katika kundi lao kwa alama 7 sawa na Canada iliyomaliza ya pili lakini kwa uchache wa mabao.

Ghana nayo iliyokuwa imejumuishwa katika kundi moja na Ujerumani, China na Uruguay ilimaliza ya pili kwa alama 6 katika kundi lao.

Mataifa mengine ambayo pia yamefuzu katika hatua hiyo  ni pamoja na Korea ,Canada Brazil ,Japan na Ufaransa.

Mechi za robo fainali zitakazochezwa siku ya Alhamisi, Nigeria itacheza na Ufaransa, Korea ichuane na Canada, Ujerumani na Brazil huku Japan ikimenyana na Ghana.

Gambia ambayo pia iliwakilisha bara la Afrika katika michuano hiyo ilimaliza ya mwisho baada ya kufungwa mechi zao zote.

Fainali itachezwa wiki ijayo.