Cricket

Uingereza yaishinda Australia kumenyana na New Zealand katika michuano ya Twenty20 ya Cricket

Timu ya taifa ya Uingereza ya mchezo wa Cricket kwa upande wa akina dada imeishinda Australia kwa wiketi saba na kufuzu katika awamu ya nusu fainali ya michuano ya kimataifa ya twenty20 inayoendelea nchini Sri lanka.

Matangazo ya kibiashara

Uingereza sasa itamenyana na New Zealand siku ya Alhamsi katika hatua hiyo baada ya ushindi huo ambao kwa kiasi kikubwa Australia walikuwa wanapewa nafasi kubwa kushinda kwa alama 145 baada ya kuanza vizuri kwa kupata mikimbio 39 kutoka kwa kurusha kwa mipira 31.

Licha ya kushindwa, Australia wamesonga mbele na watamenyana na West Indies katika mchuano mwingine wa nusu fainali siku ya Ijumaa kabla ya fainali kuchezwa siku ya Jumapili.

Kwa upande wa wanaume, mchezaji wa Uingereza Kevin Pietersen anatarajiwa kurejea tena katika kikosi cha Uingereza kwa muda wa siku mbili zijazo baada ya kuomba radhi kwa kutuma ujumbe wa kukera kudai kuwa  hataichezea tena nchi yake  kutokana na kutojumuishwa kwake  katika kikosi cha Uingereza kilichocheza nchini Afrika Kusini mwezi wa nane.

New Zealand wameondolewa katika michuano hiyo baada ya kufungwa na West Indies  kwa alama 139.