michezo

Andy Murray aboronga katika michuano ya wazi Japan baada ya kukubali kichapo cha Milos Raonic

Mcheza tennis mashuhuri duniani Andy Murray ambaye ameshindwa katika michuano ya wazi ya Japan
Mcheza tennis mashuhuri duniani Andy Murray ambaye ameshindwa katika michuano ya wazi ya Japan REUTERS/Adam Hunger

  Bingwa mtetezi Andy Marry amepoteza katika michuano ya wazi inayofanyikia huko Japan kwa kutwangwa na mpinzani wake Milos Raonic kwa seti za 6-3, 6-7 ,5-7, 7-6 ,7-4.

Matangazo ya kibiashara

Andy Murray ameboronga alama za mechi mbili baada ya kupoteza katika michuano ya nusu fainali za wazi za Japan ambapo Milos Raonic alimtoa kwa seti tatu.

Ushindi wa Raonic dhidi ya Andy katika ufunguzi wa michuano hiyo unamuweka pazuri kwa rekodi za 6-3 6-7 (5-7) 7-6 (7-4).

Naye mchezaji Marcos Baghdatis kutoka Cyprus atakutana na raia wa Japan Kei Nishikori katika michuano mingine ya nusu faiali.

Hapo awali Andy alifikia hatua hiyo baada ya kumshinda bingwa nambari 16 Stanislas Wawrinka ingawa alipoteza katika mchezo wake wa awali.