Cote D' Ivoire

Didier Drogba asifu mchezo wa soka kuunganisha Cote D' Ivoire baada ya vita

Mark Kolbe/Getty Images

Mchezaji wa kimataifa wa Cote D' Ivoire Didier Drogba amesema kuwa mpira wa miguu ni chombo pekee cha kinachowaunganisha wananchi wa nchi yake iliyowahi kukumbwa na vita.

Matangazo ya kibiashara

Drogba amesema kuwa timu ya taifa ya nchi hiyo ina umuhimu mkubwa katika kuinganisha nchi na unatumika kama jeshi la kuwaunganisha watu wa Cote D' Ivoire.

Adha amesema kwamba mpira wa miguu una manufaa makubwa kwa sababu hata timu ya taifa inajumuisha na kuyaunganisha makabila yote kwa kuw na wachezaji kutoka kwenye makabila hayo kama vile Baoules, Betes na mengine.

Amesema kuwa nchini mwake kuna michezo mingi lakini soka linaonekana kuwa na mchango mkubwa wa kuinganisha nchi katika maisha ya kila siku.

Drogba mwenye umri wa miaka 34 alijiunga na timu ya Shanghai Shenhuaya China akitokea Chelsea ya Uingereza amesema kuwa hivi sasa mambo yamedilika kwa kiasi kikubwa tofauti na kile kipindi cha vurugu na machafuko.

Hata hivyo mchezaji huyo ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Cote D' Ivoire amesema kuwa itakuwa ni ndoto kwa timu yake kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014.

Timu ya Cote D' Ivoire Oktoba 13 inakabiliwa na mchezo wake na Senegal wa kuwania kufuzu kombe la Mataifa ya Africa za mwaka 2013 nchini Afrika Kusini.