SOMALIA-UGANDA

Kikosi Cha Timu ya Taifa ya Somalia kuweka kambi Uganda kabla ya Mashindano ya Kombe la CECAFA

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Somalia ambacho kitapiga kambi nchini Uganda kabla ya Kombe la CECAFA

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Somalia ambacho kimetangazwa kinatarajiwa kupiga kambi nchini Uganda kuanzia tarehe 8 Novemba kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Kombe la Afrika Mashariki na Kati CECAFA maarufu kama Chalenji. Kikosi cha Timu ya Taifa ya Somalia kitaweka kambi hiyo ya siku kumi na tano huko Kampala kabla ya kuanza kwa mashindano ya CECAFA ambayo yanaandaliwa na Uganda mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Nchini Somalia Abdi Qani Said Arab amesema kile ambacho kimewafanya kuweka kambi nchini uganda ni kutokana na kukosa Uwanja kutokana na ule waliokuwa wanautumia kuwa kwenye ukarabati.

Said Arab ameweka bayana Uwanja wao wa zamani ambao walikuwa wanautumia kwa sasa upo kwenye matengenezo ambayo yanagharamiwa na Shirikisho la Soka Duniani FIFA kwa hiyo hawana sehemu nyingine ya kufanyia mazoezi.

Katibu Mkuu huyo wa SFF amesema licha ya kuwepo sababu nyingine nyingi lakini kitu kikubwa na tofauti ya hali ya hewa kati ya Uganda na Somalia hivyo wataenda mapema ili kuzoea hali hiyo.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa SFF Said Arab amekiri uwanja wao mwingine kutumia kama kambi ya Majeshi ya Umoja wa Afrika Yanayolinda Amani AMISOM hivyo kutatiza maandalizi yao.

Kikosi cha Somalia kinajumuisha wachezaji saba ambao wanasakata Soka ya kulipwa nje ya Taifa hilo wakiwemi wawili wanaocheza nchini Uingereza, wengine wawili wanasakata kabumbu Marekani huku wawili wakicheza Uholanzi na mmoja Kuwait.

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Somalia kitaweka kambi hiyo ya siku kumi na tano huko Kampala kabla ya kuanza kwa mashindano ya CECAFA ambayo yanaandaliwa na Uganda mwaka huu.