COTE D'IVOIRE

Lamouchi apania kufuata nyayo za Mourinho katika kuinoa Cote d'Ivoire

Kocha mkuu wa Cote d'Ivoire Samri Lamouchi akimuelekeza jambo nyota wa soka Didier Drogba katika mafunzo ya kukinoa kikosi cha Taifa
Kocha mkuu wa Cote d'Ivoire Samri Lamouchi akimuelekeza jambo nyota wa soka Didier Drogba katika mafunzo ya kukinoa kikosi cha Taifa REUTERS/Thierry Gouegnon

Kocha mkuu wa Cote d'Ivoire Sabri Lamouchi yupo nchini Uhispania katika ziara muhimu ya kimichezo yenye lengo la kuona jinsi klabu ya Real Madrid inavyopata mafunzo chini ya mkufunzi wake mkuu Jose Mourinho.

Matangazo ya kibiashara

Lamouchi ambaye ni mchezaji wa zamani katika klabu za Inter Milan, Parma na Marseille amesema anafurahia ziara hiyo ya kuangalia mafunzo yanayotolewa na Mourinho ambaye ni kocha bora na klabu anayoinoa ni bora duniani.

Lamouchi pia atatumia ziara hiyo pia kutazama mechi kati ya Real Madrid na Borussia Dortmund itakayopigwa jumanne hii katika mwendelezo wa mechi za mabingwa barani Uropa.

Lamouchi mwenye umri wa miaka 40 anajivunia kukinoa kikosi cha Cote d'Ivoire kutokana na kuwa na wachezaji nyota wanaoshika chati katika ulimwengu wa zoka kwani wanachezea klabu za kimataifa.

Wadau wa masuala ya michezo wanaona kuwa ziara hiyo ni muhimu katika wakati huu ambapo Cote d'Ivoire inajiandaa na mashindano ya kombe la bara la Afrika katika kundi D ambalo linalotajwa kuwa gumu zaidi kwani linajumuisha vigogo wa soka ambao ni pamoja na Togo, Algeria na Tunisia.