SOKA-ULAYA

Olympiakos na Montpellier kukabiliwa na adhabu

Olympiakos wakipambana na Montpellier
Olympiakos wakipambana na Montpellier stamfordadvocate.com

Shirikisho la soka barani Ulaya EUEFA limesema kuwa timu za Olympiakos Piraeus na Montpellier zitafikishwa kizimbani kutokana na vurugu zilizotokea wakati wa mtanange wa ligi ya mabingwa baina ya timu hizo siku ya Jumanne. 

Matangazo ya kibiashara

Timu ya Olympiakos ya nchini Ugiriki inakabiliwa na tuhuma za kutumia mihimili ya taa dhidi ya wachezaji na mashabiki wao, kurusha milipuko wakati wa mchezo huo na kwamba timu ya Montpellier yenyewe inakabiliwa na tuhuma za kusababisha usumbufu kwa umma, kurusha na kuwasha moto.

Ripoti za vyombo vya habari zinaarifu kuwa mashabiki wapatao 100 wa timu ya Montpellier walikabiliana na polisi wa kutuliza ghasia kabla ya mchezo wa kundi B.

Aidha shirikisho hilo limeongeza kuwa timu ya Olympiakos huenda ikakabiliwa na tuhuma za utovu wa nidhamu, madai ambayo huipata timu yoyote inapopata kadi za njano tano aua zaidi.

Shutuma dhidi ya timu hizo mbili zitasikilizwa mnamo Novemba 22.

Katika mchezo huo timu ya Olympiakos Piraeus ikiwa nyumbani iliichakaza timu ya Montpellier kwa magoli matatu kwa moja.