UINGEREZA

Novak Djokovic amshikisha adabu Roger Federer na kutwaa ubingwa ATP

REUTERS/Suzanne Plunkett

Mashabiki wa mchezo wa tennis wanasherekea ubingwa wa Novak Djokovic alioupata katika michuano ya tenisi ya ATP Tour, nyota huyo ameweka wazi kuwa ushindi alioupata utakuwa ni tuzo ya heshima kwa baba yake mzazi ambaye kwa sasa ni mgonjwa.

Matangazo ya kibiashara

Djokovic anaamini kuwa tuzo hiyo itamfariji baba yake Srdjan na sasa yupo katika mchakato wa kwenda Serbia kumjulia hali mzazi wake huyo na pia kuwasilisha nyumbani tuzo aliyoitwaa katika msimu huu.

Djokovic ametwaa ubingwa wa ATP Tour msimu huu baada ya kumbwaga mpinzani wake Roger Federer licha ya changamoto nyingi zilizokuwa zikimuandama.

Ushindi wa seti 7-6, 8-6 na 7-5 ulitosha kumfanya raia hiyo wa Serbia kuibuka bingwa wa ATP Tour msimu huu na kumfanya kuendeleza historia safi ya ushindi alioupata mwezi january mwaka huu katika michuano ya wazi ya Australia.

Mpaka kutinga katika fainali hizo Djokovic alifanikiwa kuwabwaga Andy Murray na Juan Martin del Potro katika michuano ya juma lililopita hatua ambayo imempa hamasa zaidi na ameahidi kuendeleza jitihada zaidi katika kupeperusha bendera ya mchezo wa tennis duniani.