AFRIKA KUSINI

Upasuaji wamlazimu Ntlhe kutochezea Bafana Bafana baada ya kuumia goti

RFI

Mlinzi wa klabu ya Peterborough United ya Afrika kusini defender Kgosi Ntlhe atapumzika kucheza mechi kwa takribani miezi minne baada ya kutakiwa kufanyika upasuaji wa kifundo cha goti.

Matangazo ya kibiashara

Kitendo cha kuumia kwa mchezaji huyo kinaondoa matumaini kwa mchezaji huyo kushiriki katika kikosi cha Bafana Bafana kitakachopeperusha bendera ya Afrika kusini katika michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2013.

Kocha wa timu ya taifa ya Afrika kusini Gordon Igesund amethibitisha taarifa za kutokuwepo kwa mchezaji huyo katika kombe la mataifa kutokana na majeraha ya mguuni kuendelea kumsumbua jambo ambalo linaweza kuchangia kupumzishwa kwa mchezaji huyo.

Taratibu zinafanyika ili mchezaji Ntlhe mwenye umri wa miaka 18 akafanyiwe upasuaji wa kifundo cha goti na endapo hali yake kiafya itarejea salama huenda akarudi mwanzoni mwa mwezi wa nne mwaka juao.

Kukosekana kwa Ntlhe kwa muda huo atakaokuwa akifanyiwa upasuaji kumetajwa kuwa pigo kwa klabu yake kutokana na matarajio mazuri yaliyokuwepo kwa kijana huyo mwenye uwezo mkubwa katika kandanda ikizingatiwa kuwa klabu kadhaa za huko Uingereza ziliripotiwa kuguswa na hamasa za Ntlhe.

Majeraha hayo yamechangia kutoshiriki kwa mchezaji huyo katika kikosi cha Bafana Bafana katika michuano ya mataifa ya Afrika mwaka 2013 ambayo yatafanyika nchini humo kuanzia 19 January na 10 February.