michezo

Serengeti boys ya Tanzania kuumana na Congo Brazzaville jumapili

Serengeti Boys ya Tanzania ambayo iko chini ya Kocha Jakob Michelsen itacheza mechi dhidi ya Congo Brazzaville kesho
Serengeti Boys ya Tanzania ambayo iko chini ya Kocha Jakob Michelsen itacheza mechi dhidi ya Congo Brazzaville kesho janejohn5.blogspot.com

Mechi ya raundi ya mwisho ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 kati ya Tanzania Serengeti Boys na Congo Brazzaville inatarajiwa kupigwa jumapili Novemba 18 mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Mashabiki wa kandanda kote Afrika mashariki na kati wanangojea kwa hamu mechi hiyo itakayochezwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Tayari kikosi cha Congo Brazzaville kimeshatua jijini Dar es salaam tayari kwa kipute hicho cha jumapili cha mchujo wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17.

Serengeti Boys inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa chini ya Kocha wake Jackob Michelsen wakati kikosi cha Congo Brazzaville ambacho katika raundi ya pili kiliitoa Zimbabwe kitafanya mazoezi yake ya mwisho Jumamosi jioni kwenye Uwanja wa Taifa.

Makocha wa timu zote mbili na manahodha wao watakutana na waandishi wa habari Jumamosi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuzungumzia maandalizi yao kwa ajili ya mechi hiyo kabambe.