UINGEREZA

Manchester City yakiri kumkosa Van Persie kumeharibu mbio zao za ubingwa msimu huu

Mshambuliaji wa Manchester United Robin Van Persie ambaye Manchester City wanahuzunika kwa kushindwa kumsajili
Mshambuliaji wa Manchester United Robin Van Persie ambaye Manchester City wanahuzunika kwa kushindwa kumsajili

Klabu ya Manchester City imekiri hatua ya kukosa kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Arsenal anayekipiga katika Klabu ya Manchester United Robin van Persie inaweza ikawagharimu katika mbio zao za kutetea ubingwa msimu huu. Kocha Mkuu wa Manchester City Roberto Mancini amesema kumkosa Van Persie imekuwa ni kosa kubwa kwao kutokana na umahiri wa mshambuliaji hayo katika uwezo wake wa ufungaji magoli.

Matangazo ya kibiashara

Mancini amekiri Robin van Persie amekuwa muhimu sana kwa Manchester United msimu huu kutokana na kufunga magoli 14 katika michezo yake 20 ya ligi kitu kinachowafanya kuwa kileleni mwa Ligi.

Kocha Mancini amesema miezi mitatu au minne kabla walikuwa karibu kabisa kumnasa Van Persie lakini hatua za mwishoni mambo yakabadilika na hivyo wakajikuta wakimkosa mshambuliaji huyo.

Mancini anasema tofauti ya pointi saba baina yao na Manchester United imechangiwa kwa kiasi kikubwa na kusajiliwa kwa Van Persie ambaye amekuwa akifunga magoli muhimu kwenye kila mchezo.

Manchester City imeeleza Van Persie ni mshambuliaji muhimu sana na kama angepatikana basi angesaidia washambuliaji kuweza kufunga magoli mengi tofauti na ilivyo kwa sasa ambayo wanakabiliwa na tatizo la ufunguzi.

Mancini amesema alifurahishwa na namna ambavyo Manchester City walivyocheza vizuri kwenye eneo la ushambuliaji akiwatumia Sergio Aguero, Carlos Tevez, Edin Dzeko na Mario Balotelli.

Manchester City imeonekana kuwa na safu butu ya ushambuliaji tofauti na ambavyo walikuwa wanafunga magoli msimu uliopita kitu ambacho kimeonekana kumkatisha tamaa Mancini.