UINGEREZA

Michu na Ghaham wa Swansea wapeleka kilio Chelsea

Timu ya Swansea ikiwa uwanjani
Timu ya Swansea ikiwa uwanjani

Klabu ya soka ya Swansea nchini Uingereza imeifunga Chelsea mabao 2 kwa 0 kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 87 katika mchuano wa kwanza wa nusu fainali ya michuano ya Capital One. 

Matangazo ya kibiashara

Washambulizi Miguel Michu na Danny Graham ndio waliowapa ushindi Swansea katika dakika ya 39 na 90 ya mchuano huo katika uwanja wa nyumbani wa Chelsea wa Stamford Bridge licha ya kuutawala.

Michu ambaye alisalijiwa kutoka klabu ya Rayo Vallecano ya Uhispania ameifungia Swansea bao la 16 katika klabu yake.

Bao la Demba Ba katika dakika za lala salama lilikataliwa baada ya kubainika kuwa alikuwa ameotea.

Ushindi wa Sweasea umewapeleka katika awamu ya pili ya nusu fainali ya michuano hiyo tarehe 23 mwezi huu wa Januari katika uwanja wao wa nyumbani wa Liberty wakiwa na matumai ya kunyakua taji hilo ndani ya miaka 100 .

Kocha wa Chelsea Rafael Benitez amesema wachezaji wake hawakuwa na bahati nzuri katika mchuano huo na kuahidi kufanya vizuri katika mchuano wa marudiano.

Mashabiki wa Chelsea walimzomea Benitez baada ya timu yake kushindwa kupata ushindi wakiwa nyumbani.