FA CUP-PREMIER LEAGUE-COPA DE RELAY

Chelsea yatupwa nje michuano ya Capital One, Arsenal yatamba mechi ya ligi kuu

Wachezaji wa timu ya Swansea wakishangilia baada ya timu yao kusonga mbele kwa kuiondoa Chelsea
Wachezaji wa timu ya Swansea wakishangilia baada ya timu yao kusonga mbele kwa kuiondoa Chelsea Reuters

Klabu ya Chelsea ya Uingereza imeendelea kuwa na msimu mbaya baada ya siku ya Jumatano usiku kujikuta ikitolewa kwenye michuano ya kombe la Capital One linalosimamia na chama cha soka nchini humo. 

Matangazo ya kibiashara

Chelsea imejikuta ikiaga michuano hiyo baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na klabu ya Swansea kwenye mchezo ambao mashabiki wa Chelsea waliondoka uwanjani vichwa chini.

Mchezo wa hiyo jana ulikuwa ni wamarudio ambapo kwenye mchezo wa awali timu ya Swansea ilifanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Chelsea.

Kutolewa kwa timu hiyo kumekuwa pigo jingine kwa mashabiki wa klabu hiyo ambayo mashabiki wake wanazidi kuongeza shinikizo kwa kocha Rafa Benitez kuhakikisha timu hiyo inashinda.

Katika mchezo wa Ligi kuu ya Uingereza, washika bunduki wa jiji la London klabu ya Arsenal wakitoka nyumba kwa goli moja walifanikiwa kuchomoza na ushindi mnono wa mabao 5-1 dhidi ya klabu ya Westham United.

Nchini Uhispani, michuano ya kombe la Copa Del Rey klabu ya Real Madrid imefanikiwa kusonga mbele kwenye michuano hiyo licha ya kutoka sare ya bila kufungana na timu ya Valencia, mdrid imesonga mbele kufuatia ushindi iliyoupata nyumbani.

Mechi nyingine Sevilla ilikuwa na kibarua dhidi ya Zaragoza kwenye mchezo ambao Sevilla ilifanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 4-0 na kutinga kwenye hatua ya nusu fainali.