AFCON 2013

Ghana yawa kinara kundi B, DR Congo na Niger hakuna mbabe, leo ni Zambia na Nigeria, Burkina Faso na Ethiopia

Mshambuliaji wa Ghana, Mubarak Wakaso akishangilia goli alilofunga dhidi ya Mali
Mshambuliaji wa Ghana, Mubarak Wakaso akishangilia goli alilofunga dhidi ya Mali Reuters

Mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika yanyoendelea kutimua vumbi kule nchini Afrika Kusini yamefikia kwenye hatua nzuri kufuatia baadhi ya timu kujiweka kwenye nafasi nzuri huku zingine zikisubiri mechi zao za mwisho.

Matangazo ya kibiashara

Kwenye mechi za alhamisi timu ya taifa ya Ghana ambayo ni kinara wa kundi B ilikuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Mali kwenye mchezo ambao ulikuwa mkali na wakusisimua kwa muda wote wa dakika 90.

Kwenye mchezo huo ambao awali ilikuwa vigumu kubashiri nani angeweza kuibuka na ushindi hatimaye ukame wa mabao kwenye mechi hiyo ukavunjwa baada ya Ghana kuzawadiwa Penalt katika dakika ya 38.

Penalt ya Ghana ilifungwa na mshambuliaji Mubarak Wakaso ns kuips ushindi wa kwanza timu yake na hivyo kuiwezesha kuwa kinara wa kundi B.

Katika mchezo mwingine, timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRc ilikuwa ikipepetana na timu ya taifa ya Niger kwenye mchezo mwingine ambao ulikuwa mgumu na wakusisimua kwa muda wote wa mchezo.

Mchezo huo hata hivyo haukuweza kutoa mshindi baada ya timu hizo kulazimishana sare ya bila kufungana na hivyo kufanya timu hizo kufahamu hatma zao kwenye mechi za mwisho.

Hii leo kwenye kundi C kutakuwa na mechi za kukata na shoka ambapo mabingwa watetezi wa kombe hilo timu ya taifa ya Zambia itakuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria kwenye mchezo mwingine unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka barani Afrika.

Mchezo mwingine wa kundi C utazikutanisha timu ya taifa ya Burkina Faso ambayo itakuwa ikicheza na Ethiopia kwenye mchezo ambao unatarajiwa kuwa mgumu kwa timu zote mbili kutokana na aina ya mchezo ambao timu hizo zinacheza.