Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Liverpool, Tottenham zaondolewa hatua ya Tano ya Kombe la Chama Cha Soka Nchini Uingereza FA

Mchezaji wa Oldham Matt Smith akifunga goli la kwanza dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa Kombe la FA
Mchezaji wa Oldham Matt Smith akifunga goli la kwanza dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa Kombe la FA
Ujumbe kutoka: Nurdin Selemani Ramadhani
1 Dakika

Mashindano ya Kombe la FA nchini Uingereza yameshuhudia mshtuko wa hali ya juu kutokana na Klabu za Liverpool na Tottenham Hotspur kuondolewa kwenye hatua ya nne ya mashindano hayo baada ya kupata vipigo.

Matangazo ya kibiashara

Chelsea wenyewe walinusurika kuondolewa kwenye mashindano hayo baada ya kuambulia sare ya magoli 2-2 kutoka kwa Klabu ya daraja la chini ya Brentford na sasa italazimika kurudiana nayo ili kupata timu itakayofuzu.

Liverpool imeondoshwa kwenye masindano hayo baada ya kujikuta ikiambulia kichapo cha magoli 3-2 kutoka kwa Oldham Athletic kitu ambacho kimefanya kuwa ni tukio la kihistoria katika historia ya mpira wa miguu.

Oldham ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata goli la kuongoza lakini Vijogoo vya Jiji vikafanikiwa kusawazisha goli hilo na kurejesha matumaini ya kufanya vizuri lakini wakajikuta jahazi lao linaziamishwa kwa kipigo cha magoli 3-2.

Tottenham wakiwa wamefunga safari kueleka Elland Road wakajikuta wakiondosha kwenye mashindano ya Kombe la FA kwa kufungwa magoli 2-1 na wenyeji wao Leeds United.

Leeds ambao walikuwa wanacheza kwa kujiamini walifanikiwa kujipatia magoli yote mawili kitu ambacho kiliwapa wakati mgumu Tottenham ambao walifanikiwa kupata goli la kufutia machozi.

Kwa matokeo hayo sasa Leeds watalazimika kufunga safari kuwafuata Manchester City kwenye hatua ya tano huku Manchester United wakitarajiwa kuwaalika Reading kwenye dimba la nyumbani la Old Trafford.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.