Michezo-AFCON

Nigeria kupambana na Burkina Faso huku Ghana ikichuana na Mali katika nusu fainali ya Afcon nchini Afrika Kusini

Kindumbwe ndumbwe jioni hii katika michuano ya kombe la mataifa barani Afrika huko nchini Afrika Kusini ambapo Mali itachuana na Nigeria katika nusu fainali ya michuano hiyo, wakati Ghana ikipepetana na BurkinaFaso.

Mashabiki wa Ghana wakishangilia timu yao wakati wa mazoezi huko Port Elizabeth
Mashabiki wa Ghana wakishangilia timu yao wakati wa mazoezi huko Port Elizabeth REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Ghana ilikutana na Mali katika mzunguuko wa kwanza na Ghana ikabeba ushindi dhidi ya Mali kufuatia mkwaju wa penalti ambapo timu hizo zilikuwa zimetoshana nguvu ya sufuri kwa sufuri.

Nigeria tayari imeshawahi kutwa kombe hilo mara tatu, huku Mali ikiwa tayari imesha cheza fainali ya kombe hilo mara mbili bila kutwa kombe.

Kocha wa timu ya Nigeria Stephen Kechi amesema kuwa timu yake inao wachezaji wazuri wenye uwezo wa kufika fainali ya michuano.

Wakati huo huo Ghana ambayo tayari imetwa kombe hilo mara nne itakutana na Burkinafaso.

Mechi kati ya Mali na Nigeria itapigwa jijini Durban, saa kumi na mbili jioni majira ya Afrika Mashariki Afrika ya kati itakuwa ni saa kumi na moja, huku BurkinaFaso na Ghana ikipigwa jijini Nelspruit saa mbili na nusu majira ya Afrika mashariki wakati Afrika ya kati ni saa moja na nusu.