Michezo-AFCON

Kocha wa Nigeria atangaza nia yake ya kuachia ngazi wakati Burkina Faso ikisubiri uamuzi wa CAF juu ya kadi nyekundu aliopewa mchezaji wake

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Nigeria Stephen Keshi anayefahamika kwa jina maarufu kama the big boss amejitokeza na kuelezea sababu zake za kutaka kuacha kazi baada ya fainali ya kombe la mataifa bingwa barani Afrika siku ya Jumapili dhidi ya Burkinafaso.

Kocha mkuu wa Nigeria Stephen Keshi
Kocha mkuu wa Nigeria Stephen Keshi Reuters/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Keshi aliwaashangaza wapenzi wa soka alipotoa tangazo hilo huko Durban akisema kuwa wengi wa wananchi wa Nigeria hawaoni juhudi anazofanya kuingoza timu hiyo.

Keshi ambaye pia amewahi kuifunza Togo na Mali alitofautiana na viongozi wa soka wa Nigeria NFF baada ya kutoka sare ya bao 1 kwa 1 na Burkinafaso katika mzunguuko wa makundi.

Hayo yanajiri wakati Burkina Faso ikisubiri ripoti kutoka kwa shirikisho la soka barani Afrika CAP kuhusu hatma ya mshambuliaji wake Jonathan Pitroipa aliepewa kadi nyekundu wakati wa mchuano wa nusu fainali na Ghana katika dimba la mataifa bingwa barani Afrika.

Burkina Faso ilikata rufaa kwa CAF kulalamikia hatua ya refarii Slim Jdidi kutoka Tunsia anayetuhumiwau kumpa Pitroipa kadi nyekundu.

Tayari CAF imempiga marufuku refarii Djidi huku ikitarajiwa kutoa ripoti ya mwisho kumhusu.

Burkinafaso iliyoishinda Ghana mabao 3 kwa 2 kupitia mikwaju ya Penalti itacheza na Super Eagles ya Nigeria katika fainali siku ya jumapili huko Johanesburg.