SOKA

Ferguson asema hatima ya taji la soka nchini Uingereza mikononi mwa wachezaji wake

Kocha wa klabu ya soka ya Manchester United nchini Uingereza Alex Ferguson amekiri kuwa hatima ya timu yake kunyakua ubingwa wa taji kuu la soka nchini humo liko mikononi mwa wachezaji wake.

Matangazo ya kibiashara

Ferguson ameyasema hayo baada ya wachezaji wake kuishinda klabu ya Everton kwa mabao 2 kwa 0 mwishoni mwa juma lililopita .

Ushindi huo wa United unaifanya iendelee kuongoza msururu wa ligi kuu nchini humo kwa alama 65 mbele ya Manchester City iliyo na alama 53 na kutofautisha timu hizo mbili kwa alama 12.

Hata hivyo, Ferguson amesema kuwa hawezi kuidharau Manchester City kwa sababu bado kuna mechi 12 za kuchezwa kabla ya kumalizika kwa msimu wa soka nchini humo na chochote kinaweza kutokea.

Ferguson amesisitiza umuhimu wa timu yake kuendelea kupata ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kunyakua taji hilo.

Manchester United inatarajiwa kumenyana na Real Madrid siku ya Jumatano katika mchuano wa klabiu bibgwa barani Afrika katika uwanja wa Bernabeu.