SOKA

Manchester United na Real Madrid kutoana kijasho mchuano wa UEFA

Klabu tajiri ya soka duniani Real Madrid kutoka Hispania inashuka dimbani Jumatano usiku kumenyana na Manchester United kutoka Uingereza katika mchuano wa klabu bingwa barani Ulaya UEFA baina ya vlabu 16 bora.

Matangazo ya kibiashara

Kocha wa Real Madrid Jose Mourihno amesema huu ndio mchuano ambao dunia inasubiri kushuhudia kutokana na ubora wa vlabu hivi viwili katika ligi zao.

Manchester United watakuwa ugenini huko Madrid katika uwanja wa Santiago Bernabeu baada ya kuendeleza matokeo bora katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza kwa kuichabanga Everton mabao 2 kwa 0 na kujitenga na wapinzani wao Manchester City kwa alama 12.

Real Madrid nayo itacheza mechi hii ikiwa nyuma alama 16 dhidi ya Barcelona katika msururu wa ligi ya La Liga nchini Uhispania na matokeo mabaya msimu huu yakielezwa ni kutokana na maneno makali kati ya Mourihno na wachezaji wake.

Miongoni mwa wachezaji watakaokuwa wanategemewa sana kwa upande wa Real Madrid ni pamoja na chipukizi Raphael Varane na Ricardo Carvalho ambaye amekuwa na ushawishi na uzoefu mkubwa katika klabu hiyo.

Manchester United nayo itakuwa inawategemea sana Rio Ferdinand, Michael Carrick, Ashley Young na Shinji Kagawa ambao walipumzishwa wakati wa mchuano wa mwisho wa juma lililopita.

Mchunao mwingine utakaochezwa ni kati ya Shaktar Donestsk dhidi ya Borrussia Dortmund huku Jumanne usiku Celtic ya Scotland itakuwa nyumbani kumenyana na Juventus ya Italia huku Valencia ikimemaliza kazi na Paris SG ya Ufaransa.