Miereka

Japan yalilia mchezo wa Miereka urudishwe wakati wa michezo ya Olimpiki 2020

Bingwa wa mchezo wa Miereka duniani Japan, iliyopata medal nne za dhahabu katika mchezo huo wakati wa michuano ya Olimpiki iliyofanyika mwaka uliopita jijini London Uingereza inasema imesikitishwa sana na hatua ya viongozi wa michezo ya Olimpiki kuondoa mchezo huo wakati wa michezo ya Olimpiki mwaka 2020.

Matangazo ya kibiashara

Saori Yoshida mchezaji ambaye ameishindia Japan medali 13 katika mashindano hayo kwa kipimdi cha miaka 10 iliyopita amesema hatua hiyo imemshtua na ni  kama imekatiza ndoto yake ya kunawiri zaidi katika mchezo huo.

Hatua ya kuondoa mchezo huo katika michezo ya Olimpliki iliamuliwa na wanachama 15 wa Kamati ya Kimataifa ya michezo ya Olimpiki lakini bado haijapitiswa na wanachama wote wa shirikisho hilo.

Hata hivyo, mchezo huo utasalia katika mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2016 nchini Brazil baada ya kuanza kuchezwa wakati wa mwaka wa 708 BC na kukosa tu mara moja wakati wa mashindano ya Olimpiki mwaka wa 1900.

Chama cha kimataifa cha wachezaji chipukizi wa mchezo huo nacho kimeonesha masikitiko makubwa  kuhusu uamuzi huo na kimesema kitakuwa kinapata maelezo ya kina ni kwanini mchezo huo umeondolewa katika michezo hiyo ya Olimpiki.

Naye rais wa shirikisho la mchezo huo nchini Urusi Mikhail Mamiashvili amesema hatari ya mchezo huo inaonekana ikiwa utaruhusiwa wakati wa mashindano hayo  ya  Olimpiki mwaka 2020.

Mchezo wa miereka sasa utakuwa unajadiliwa na wadau wa Kamati ya Olimpiki ikiwa utarudishwa katika michezo hiyo pamoja na ule wa Squash, Baseball na Karate.