TENNIS

Rafael Nadal amshinda Martin Alund katika nusu fainali za michuano ya wazi ya Brazili

REUTERS/Toby Melville

Rafael Nadal ameonyesha ubingwa wake katika mchezo wa tennis na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa seti tatu dhidi ya Loser Martin Alund wa Argentina katika nusu fainali za michuano ya wazi ya Brazili.

Matangazo ya kibiashara

Nadal ambaye amewahi kuwa kinara namba moja wa mchezo huo duniani kwa upande wa wanaume aliibuka na ushindi wa seti 6-3, 6-7(2/7), 6-1 dhidi ya Alund ambaye kwa sasa yupo katika nafasi ya 111 katika ubingwa wa mchezo huo duniani.

Nadal ambaye anawania kutwaa ubingwa wa michuano ya wazi ya Brazili mwaka huu mwaka 2005 alilalamikia kukabiliwa na maumivu ya goti baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa jumamosi.

Fainali ya jumapili hii itamkutanisha Nadal na David Nalbandian wa Argentina ambaye aliibuka na ushindi dhidi ya Simone Bolelli kwa seti 6-3, 7-5 katika dakika 85 za michuano mingine ya nusu fainali.

Hii itakuwa ni fainali ya pili kwa Nadal tangu aliporejea baada ya kuwa nje kwa miezi saba kutokana na kukabiliwa na majeraha katika goti lake la kushoto.