TENNIS

Rafael Nadal ashinda Taji la kwanza katika kipindi cha miezi saba la Brazil Open

Rafael Nadal akiwa na Taji lake la Brazil Open baada ya kumfunga David Nalbandian huko Sao Paulo
Rafael Nadal akiwa na Taji lake la Brazil Open baada ya kumfunga David Nalbandian huko Sao Paulo

Mcheza Tennis mahiri Duniani Rafael Nadal hatimaye ameshinda Taji lake la kwanza baada ya kukaa nje kwa miezi saba kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti yaliyomfanya asishiriki mashindano kadhaa. Nadal kwa mara ya mwisho alishinda Taji la French Open hapo mwaka jana kisha akakutwa na jinamizi la kuumia mara kadhaa lakini ameibuka kwenye Brazil Open na kuibuka mshindi wa mashindano hayo.

Matangazo ya kibiashara

Mchezaji huyo aliyekuwa anashika nafasi ya kwanza ulimwenguni kwa upande wa wanaume alitwaa taji hilo baada ya kumfunga David Nalbandian kwenye mchezo wa fainali uliokuwa wa kuvutia.

Nadal hakupata upinzani mkubwa kwenye mchezo huo baada ya kushinda seti zote mbili kwa 6-2 na 6-3 na hivyo kumaliza ukame wake wa kukosa mataji kwa kipindi cha miezi saba alichokuwa anauguza jeraha.

Mchezo wa fainali ulipigwa katika Jiji la Sao Paulo na kuchukua muwa saa 1 na dakika 18 kabla ya kumalizika ambapo seti ya pili Nadal alipata upinzani baada ya Nalbandian kuongoza kwa 3-0 kabla ya kufungwa yeye.

Nadala baada ya kuibuka na ushindi hakusita kueleza hisia zake ya kwamba hu ni mwanzo mzuri kwa upande wake baada ya miezi saba kuwa nje kutokana na mauamivu na sasa anaimani atafanya vizuri.

Mashindano yajayo kwa Nadal ni yale ya Mexican Open ambayo yataanza tarehe 25 Februari huku mwenyewe akielekeza nguvu zake kuchukua taji la nane la Franch Open katika mchuano utakaoanza mwezi Juni.