UINGEREZA

Manchester United yatinga Robo Fainali ya Kombe la FA baada ya kuifunga Reading

Klabu ya Manchester United imefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Chama Cha Soka nchini Uingereza FA baada ya kuvuna ushindi wa magoli 2-1 mbele ya Reading. Magoli ya Luis Almeida Nani na Javier Hernandez yalitosha kuwavusha Manchester Unite kutinga hatua ya Robo Fainali kwenye mchezo uliopigwa kwenye Dimba la nyumbani la Old Trafford.

Mshambuliaji wa Manchester United Luis Nani akishangilia goli lake dhidi ya Reading kwenye mchezo wa Kombe la FA
Mshambuliaji wa Manchester United Luis Nani akishangilia goli lake dhidi ya Reading kwenye mchezo wa Kombe la FA
Matangazo ya kibiashara

Wageni Reading walipata goli lao la kufutia machozi dakika tisa kabla ya kumalizika kwa mchezo kupitia kwa Jobi McAnuff na hivyo kufufua matumaini ya huenda wangesawazisha lakini mambo hayakuwa hivyo.

Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson alilazimika kufanya mabadiliko kwenye kikosi chake kilichocheza na Real Madrid kwa kuwapumzika wacheza kadhaa akiwemo Wayne Rooney, Rio Ferdinand, Robin Van Persie, Rafael Da Silva na Patrice Evra.

Wachezaji wengine ambao walipumzika kwenye mchao huo wa jana ni pamoja na Johnny Evans, Michael Carrick na Shinji Kagawa ikiwa ni mkakati wake wa kupumzisha wachezaji na kuwatumia wengine kwenye kikosi chake.

Nani ndiye aliyeleta mabadiliko kwenye mchezo huo baada ya kuingia katika dakika ya 42 kuchukua nafasi ya Phil Jones aliyetolewa baada ya kupata maumivu na hivyo kusaidia kuongeza mashambulizi ya Manchester United.

Manchester United waliutawala zaidi mchezo huo katika kipindi cha kwanza na hata cha pili kabla ya dakika kumi za mwisho Reading kuonekana kuamka na kusaka goli la kusawazisha kwa nguvu lakini waligonga mwamba.

Baada ya mchezo huo Kocha wa Manchester United Sir Ferguson amesema walikuwa na nafasi ya kufunga magoli zaidi lakini tatizo kubwa lilikuwa ni kuridhikwa kwa wachezaji wake ndiyo maana matokeo yakwa 2-1.

Naye Kocha wa Reading Brian McDermott amesema wameweza kutoa upinzani kwa klabu tajiri kama Manchester United yenye wachezaji mahiri mfano wa Robin Van Persie lakini wamecheza vizuri na amefurahishwa na kiwango.

Manchester United inasubiri mshindi kati ya Chelsea na Middlesbrough ili aweze kukabiliana naye katika hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Chama cha Soka nchini Uingereza FA.