USWISS-FIFA

FIFA yatangaza kuanza kutumia teknolojia ya kubaini mpira umevuka mstari wa goli kwenye Kombe la Dunia

Shirikisho la Soka Duniani FIFA limethibitisha rasmi litatumia teknolojia ya kutambua iwapo mpira umevuka mstari na kuwa goli kwenye Mashindano ya Kombe la Dunia yatakayofanyika nchini Brazil mwa 2014. Tangazo hilo la FIFA limekuja baada ya kuona mafanikio ya teknolojia hiyo kwenye Mashindano ya Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia yaliyofanyika nchini Japan mwezi Desemba mwaka jana.

Teknolojia hiyo ingeweza kusaidia goli lililokataliwa la Frank Lampard kwenye mchezo wao dhidi ya Ujerumani kwenye Kombe la Dunia 2010
Teknolojia hiyo ingeweza kusaidia goli lililokataliwa la Frank Lampard kwenye mchezo wao dhidi ya Ujerumani kwenye Kombe la Dunia 2010
Matangazo ya kibiashara

FIFA imesema matumuzi ya teknolojia hiyo ya kumaliza utata wa mpira kuvuka mstari wa goli au la yataanza pia kwenye Kombe la Mabara ambalo huwa linafanyika mapema kabla ya Kombe la Dunia.

Matumizi hayo ya teknolojia yakianza kwenye Kombe la Dunia itakuwa ni mafanikio makubwa kwa Rais wa FIFA Sepp Blatter ambaye amekuwa akihaha kuhakikisha mfumo huo mpya unaanza kutumika.

FIFA imetangaza zabuni kwa makampuni kuhakikisha yanatengeza teknolojia hiyo kabla ya wao hawajaamua kampuni gani ndiyo itatumika kwenye Kombe la Dunia huko Brazil mwaka 2014.

Taarifa ya FIFA imeeleza baada ya kufanikiwa kwa teknolojia hiyo kwenye Mashindano ya Kombe Klabu Bingwa ya Dunia hivyo huu ni wakati muafaka wa kutumia mfumo huo kwenye Kombe la Mabara na baadaye Kombe la Dunia.

FIFA kwenye taarifa yake imeeleza wameamua kutumia mfumo huo ili kuwasaidia waamuzi kuepukana na makosa na lawama za mara kwa mara katika kuamua magoli yenye utata na hivyo suluhu imepatikana.

Makampuni mawili ndiyo yameshatengeza mfumo wa teknolojia hiyo hadi sasa ambayo ni Goalref na Hawkeye na wito umeendelea kutolewa kwa makampuni zaidi kabla ya maamuzi ya mwisho hayajafanywa na FIFA kuwa watumie mfumo gani.