MAREKANI-TOUR DE FRANCE

Lance Armstrong akataa kula kiapo ili ahojiwe na Shirika la Marekani la Kupambana na Matumizi ya Dawa za Kuongeza Nguvu Udasa

Bingwa mara saba wa zamani wa Mashindano ya Baiskeli ya Tour de France Lance Armstrong
Bingwa mara saba wa zamani wa Mashindano ya Baiskeli ya Tour de France Lance Armstrong ©Reuters.

Bingwa mara saba wa zamani wa Mashindano ya Baiskeli ya Tour de France Lance Armstrong amekanusha taarifa ya kwamba amekubali kula kiapo ili aweze kufanya mahojiano ya Shirika la Marekani linalojihusisha na mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni (Usada). Armstrong amesema hakukubaliana na Usada kuwa atakula kiapo ili atoe maelezo ya namna ambavyo ametumia dawa za kuongeza nguvu na kuchangia kushinda mataji saba ya Tour de France kabla ya kunyang'anywa baada ya kukutwa na hatia ya kutumia dawa hizo.

Matangazo ya kibiashara

Bingwa huyo wa zamani wa Tour de France alikiri kutumia dawa hizo za kulevya kwenye kipindi cha Televisheni cha Oprah Winfrey lakini ameonekana kuwa mbogo pale ambapo Shirika la Usada kumtaka ale kiapo ili kueleza ukweli juu ya tuhuma zinazomkabili.

Hapo awali Armstrong alitakiwa awe amekutana na Kamati maalum ya Shirika la Udasa tarehe 6 ya mwezi Februari lakini aliongezewa majuma mawili zaidi kabla ya kufanya maamuzi kama atakuwa tayari kufanya nao mahojiano au la.

Armstrong alitangaza mapema utayari wake wa kushirikiana na Makampuni yanayofanya uchunguzi kwa wanamichezo ambao wanatumia dawa za kuongeza nguvu lakini sasa amekuwa na msimamo tofauti na kukataa kula kiapo atakapoongea na Udasa.

Mwanasheria wa Jimbo la Texas Tim Herman amesema Armstrong ameonesha utayari wake kutoa ushirikiano lakini kwa sasa hajaamua kufanya mahojiano na Shirika la Udasa ambalo limekuwa likimtaka ale kiapo wakati akitoa maelezo yake.

Herman amesema Armstrong msimamo wake bado upo wazi kuhakikisha anavisaidia vyombo mbalimbali duniani ambavyo vitakuwa vinasaka ukweli juu ya wanamichezo wanaotumia dawa za kuongeza nguvu.

Armstrong mshindi mara saba wa mbio za baiskeli za Tour de France aligonga vichwa vya habari pale alipotangaza utumiaji wake wa dawa za kuongeza nguvu na kumsababisha kushinda matahi hayo.