UINGEREZA-SOKA

Klabu ya Manchester United yakanusha madai ya kutaka kumuuza Kiungo wake Luis Nani

Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson akiteta jambo na Kiungo wake Luis Nani
Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson akiteta jambo na Kiungo wake Luis Nani

Kocha Mkuu wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema Kiungo wa Kimataifa wa Ureno Luis Carlos Almeida da Cunha maarufu kama Nani ataendelea kuwa na msimu mrefu zaidi iwapo atacheza vizuri zaidi msimu huu. Sir Ferguson ametoa kauli hiyo kutokana na uwepo wa uvumi ya kwamba Nani huenda akaondoka Manchester united kutokana na kutopewa nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza.

Matangazo ya kibiashara

Kocha huyo raia wa Scotland amesema Nani amekuwa ni mmoja wa wachezaji wanaoweza kuleta ushindi kwenye michezo ya Ulaya kutokana na kufunga magoli ya kuvutia na ya ushindi kwa Klabu yake.

Ferguson amesema kila mtu anatambua kipaji alichonacho Nani uwanjani na hivyo hawatakuwa tayari kumpoteza kama ataendelea kuwa na kiwango kizuri katika msimu huu wa ligi na mashindano mengine.

Kocha huyo wa Manchester United amesisitiza kila mtu ndani ya timu hiyo anataka kuona Nani anaendelea kuwepo kwa muda mrefu na kuendelea kuisaidia kutwa mataji aaidi katisi siku za usoni.

Nani amekuwa akiwania na klabu zenya maskani yake katika Jiji la London ambzo ni Arsenal na Tottenham lakini Sir Ferguson amewakatisha tamaa kwa kuwaeleza hawana mpango wa kumuuza kiungo huyo.

Ferguson amekataa kusema moja kwa moja kama atampa nafasi ya kudumu kwenye kikosi chake cha kwanza lakini akasema kiwango chake ndicho kitamfanya ajumuishwe kwenye kikosi hicho kutoka na uwepo wa ushindani wa namba.

Nani alionesha makali yake alipoingia kwenye mchezo wa Kombe la Chama Cha Soka Nchini Uingereza FA kwa kufunga goli la kwanza na kutengeza goli la pili dhidi ya Blackburn Rovers na kuonekana mwiba kwa mabeki wa timu hiyo.

Kiungo Nani mkataba wake na Manchester United unatarajiwa kufikia tamati mwaka 2014 huku sasa akijiweka sawa baada ya kuwa nje kutokana na kukabiliwa na majeruhi na ameanza kwenye michezo mitano pekee msimu huu.