Ufaransa

Beckham ajitoa kwa Watoto waishio katika Mazingira duni

Mchezaji wa Klabu ya Paris Saint Germain, David Beckham
Mchezaji wa Klabu ya Paris Saint Germain, David Beckham

Nahodha wa zamani wa timu ya soka ya Uingereza David Beckham hatimaye ameingia uwanjani kuichezea klabu ya Paris Sain germain ya Ufaransa dhidi ya Marseille katika mchuano wa ligi kuu nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Beckham ambaye aliingia katika kipindi cha pili cha mchuano huo dakika 16 kabla ya kumalizika kwa mchuano huo alisaidia kupatikana kwa bao la pili mchuano ambao Paris Sanuit germain walishinda kwa 2-0.

Klabu ya Paris Saint Germain inatafuta ubingwa baada ya kunyakua taji hilo kwa mara ya mwisho kabisa mwaka 1994.

Beckham yeye anasema lengo lake la kuichezea klabu hiyo ni kuwasaidia watoto wasiojiweza.

Mashabiki wa soka nchini Ufaransa walifurahishwa na Beckham kufika uwanjani wengi wakienda kutazama pasi alizokuwa akizitoa.