Uswisi

FIFA kuwafungia Watu kutojishirikisha na Soka duniani baada ya kubainika kujihusisha na vitendo vya ufisadi

Rais wa FIFA, Sepp Blatter
Rais wa FIFA, Sepp Blatter REUTERS/Stringer

Shirikisho la Soka Duniani, FIFA hii leo limesema kuwa limewafungia watu 58 kujihusisha na Mchezo wa Soka duniani kufuatia uchunguzi uliofanywa na Mamlaka ya nchini China juu ya udanganyifu kwenye mchezo wa Soka na Shutma za ufisadi.

Matangazo ya kibiashara

FIFA imesema imechukua hatua hiyo baada ya kamati ya nidhamu ya Chama cha Soka nchini Chinamwanzoni mwa kuwafungia watu 25 kutojihusisha na Mchezo wa Soka kwa miaka mitano na wengine 33 kuwafungia maisha kwa makosa ya kufanya udanganyifu.

Waliokumbwa na adhabu kutoka shirikisho la Soka nchini China ni pamoja na wakuu wa zamani wa Chama cha Soka nchini humo, Nan Yong na Xie Yalong ambao awali walikabiliwa na kifungo jela kwa makosa ya kujihusisha na vitendo vya rushwa.
 

FIFA imesema imepokea kwa mikono miwili matokeo ya uchunguzi na kuwa itafanyia kazi na kuwafungia watu hao kutojihusisha na Mchezo wa Soka popote duniani.
 

Hatua hiyo imekuja baada ya uchunguzi uliofanyika kwa miaka miwili juu ya matukio ya udanganyifu katika Mchezo wa soka uliofanyika miaka ya 90 na Mwanzoni mwa mwaka 2000.