Uhispania
Barcelona kuchuana na Real Madrid katika Mashindano ya kuwania kombe la Mfalme
Imechapishwa:
Barcelona itachuana leo usiku na watani wao wa jadi Real Madrid katika mchuano wa nusu fainali ya kuwania taji la Copa Del Rey.
Matangazo ya kibiashara
Katika mchuano wa kwanza Barcelona ilitoka sare ya 1-1 na Madrid ugenini katika uwanja wa Bernabeu.
Barcelona inacheza mchuano wa leo baada ya kufungwa na AC Milan ya Italia mabao 2- 0 katika mchuano wa kuwania taji la klabu bingwa barani Ulaya.
Huu utakuwa mchuano wa 224 kati ya timu hizi mbili.
Mshambulizi wa Barcelona Lionel Messi amesema kuwa ni sharti wachezaji wenzake watie bidii ili kupata ushindi leo usiku.