UINGEREZA

Rafael Benitez akerwa na tabia za Mashabiki wa Chelsea kumzodoa

Kocha wa klabu ya soka ya Chelsea nchini Uingereza Rafael Benitez amesema kuwa ataondoka katika klabu hiyo mwezi wa tano mwaka huu kwa kile anachokieleza hajafurahishwa anavyofahamika katika kalbu hiyo kuwa yeye ni Kocha wa muda tu. 

Kocha wa Chelsea, Rafael Benitez
Kocha wa Chelsea, Rafael Benitez REUTERS/Andrew Winning
Matangazo ya kibiashara

Benitez ambaye alionekana mwenye hasira amesema kuwa anaona ajabu kwa kuwa anaitwa yeye ni Kocha wa muda wa klabu hiyo ilhali yeye ndiye anayetoa mafunzo kikamilifu kwa wachezaji hao.

Raia huyo wa Uhispania ameongeza kuwa Mashabiki wa The Blues hawana mchango wowote katika klabu hiyo isipokuwa wameendelea kumzodoa na kumkosoa mara kwa mara.

Benitez ameyasema hayo baada ya mchuano wa taji la FA la kuwania taji la FA dhidi ya Klabu ya Middlesbrough na kushinda mabao 2 kwa 0.