JAPAN

Abe asema Tokyo itakuwa hamasa kwa mataifa mengine michuano ya Olympiki 2020

waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe
waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe businessweek.com

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, amesema kuwa Tokyo itakuwa hamasa kwa mataifa mengine endapo itapata ridhaa ya kuwa mwenyeji wa michuano ya Olympic mwaka 2020,kama ilivyokuwa mwaka 1964 baada ya kuwa nchi ya kwanza barani Asia kupata nafasi hiyo. 

Matangazo ya kibiashara

Abe amewaambia wakaguzi kutoka tume ya kimataifa ya Olympiki kuwa serikali yake itatoa ushirikiano wa kila hali kwa ajili ya jitihada za kupata kibali akiseama kwamba kuwa mwenyeji wa michuano hiyo ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu.

Timu ya wakaguzi 14 wa IOC ikiongozwa na Craig Reedie wa Uingereza, imeanza ziara ya siku nne jijini Tokyo kufanya ukaguzi wa vifaa vilivyopo na vilivyopangwa kwa ajili ya kupewa kibali cha kuwa mwenyeji wa michuano ya Olympiki mwaka 2020, ambapo pia itazulu Madrid na Istanbul baadaye mwezi huu kabla ya kuaandaa ripoti yake.