michezo ulaya

Juventus yajiapiza kutopoteza mechi yao na Celtic

Kocha wa Juventus Antonio Conte
Kocha wa Juventus Antonio Conte eurosoccerfans.com

Kocha wa klabu ya Juventus Antonio Conte amewataka vijana wake kutopoteza mwelekeo katika mechi ya robo fainali ya ligi ya mabigwa dhidi ya klabu ya Celtic hapo kesho Jumatano.

Matangazo ya kibiashara

Juventua mabayo iliichakaza Celtic kwa mabao 3-0 mwezi uliopita huko Glasgow na kuwapa wakati mgumu vijana wa Neil Lennon kufuzu katika nafasi ya nane bora.

Hata hivyo Conte amesema kuwa Juventus ambayo inawania nafasi ya nane bora kwa mara ya kwanza tangu ijiondoe mikononi mwa Aresnal mwaka 2006, amesema kuwa Celtic ni timu imara na wanajivunia hil, hivyo anaona kuwa ni lazima wazingatie mchezo baina yao kwa vile wamebakiza hatua chache kufuzu katika robo fainali.