SOKA

Ndoto ya Celtic kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya yayeyuka

REUTERS/Giorgio Perottino

Kocha wa klabu ya Juventus ya nchini Italia, Antonio Conte amepongeza hatua ya wachezaji wake kufanikiwa kuzima ndoto za klabu ya soka ya Celtic kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kuwafunga jumla ya mabao matano kwa nunge.

Matangazo ya kibiashara

Juventus sasa wamefanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa baada ya kuipata nafasi hiyo kwa mara ya mwisho mwaka 2006 ambapo walitolewa na Arsenal.

Mabao mawili ya Jeventus katika mechi ya marudiano na Celtic jumatano hii yaliwekwa kimiani na Alessandro Matri katika dakika ya 24 na Fabio Quagliarella katika dakika ya 65.

Aidha, katika mechi ya mwezi uliopita Juventus walifanikiwa kuwacharaza Celtic mabao 3-0.

Kocha wa Celtic Neil Lennon amekiri kuwa wachezaji wake walipata nafasi nzuri lakini hawakuzitumia ipasavyo, hata hivyo amesema wameonesha uwezo wao katika kuhimili changamoto za ligi ya mabingwa.