SOKA

Wayne Rooney kusalia na Manchester United msimu ujao

Shaun Botterill/Getty Images

Kocha wa klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson amesema mchezaji wa kikosi chake Wanye Rooney ataendelea kusalia klabuni hapo katika msimu ujao.

Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Ferguson imekuja baada ya kuwepo tetesi kuwa huenda safari ya mshambuliaji huyo ndani ya United imekaribia ukingoni baada ya kuwekwa benchi katika mechi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Real Madrid siku ya jumanne.

Aidha, Ferguson amethibitisha kuwa Rooney atashiriki katika mtanange wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Chelsea katika mchuano wa robo fainali wa kombe la Shirikisho.